Tanzania Bongo Flava Superstar Marioo, ametangaza rasmi jina na tarehe ya kutoka kwa albamu yake ya pili, ambayo itakuwa inaitwa TheGodSon “The God Son” au TGS kwa ufupi.
Tip of the Day - Music
The Trace Awards and Summit 2025, held in Zanzibar from February 24-26, celebrated African and Afro-descendant musical excellence, with Rema and Tyla among the winners, and featured a summit focused on the continent's creative industries.
Marioo ametangaza rasmi hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwa kuweka video fupi inayo onyesha mfano wa matukio ambayo pengine yanaweza kumtokea mtu yoyote au God Son. Kwa mujibu wa marioo albamu hiyo mpya “TGS” inatarajiwa kutoka tarehe 28 November 2024 siku ya Alhamisi.
Marioo ni moja kati ya wasanii wa bongo flava wanaofanya vizuri sana kwa sasa, huku single yake ya “Hakuna Matata” na nyingine zikiwa zimemuongezea wafuasi zaidi kwa mwaka huu 2024. Kufahamu zaidi kuhusu tracklist pamoja na wasanii walio shirikiswa kwenye Albamu hiyo mpya ya Marioo endelea kutembelea NyimboMpya.com kila siku.