Mchungaji Mashimo Aomba Kufungishwa Ndoa na Askofu Gwajima
Mchungaji Mashimo ameenda kwa Askofi Josephat Gwajima na kumuomba amfungishe ndoa na mchumba wake ambaye hakutajwa jina.
Juzi katika Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Gwajima aliwaambia waumini wake kwamba ameombwa na mchungaji Mashimo amfungishe ndoa.
“Mchungaji Mashimo amenifuata na yupo hapa, ameniomba nimfungishe ndoa. Tutamfungisha kwa sababu hili ni kanisa la watu wote,” alisema Askofu Gwajima.
Baadaye ndoa hiyo ilitangazwa kanisani hapo na Mchungaji Mashimo aliombwa kwenda mbele ya madhabahu na akamshukuru askofu huyo kwa kazi nzuri anayoifanya.
Mchungaji Mashimo amekuwa akipenda kufungishwa ndoa baada ya kumpata mchumba wake kwa siku nyingi. Hata hivyo tarehe ya ndoa hiyo haijatangazwa.
Chanzo: Global Publisher