Director Ivan Azungumzia Kuchukua Nafasi ya Director Kenny WCB — citiMuzik
Muongozaji video kutoka nchini Tanzania, Ivan hivi karibuni amekanusha tetesi zilizosambaa kuwa huenda yeye ndiye akawa director rasmi wa kampuni ya Zoom Extra inayomilikiwa na Diamond Platnumz.
RELATED: Papa Wemba Ft Diamond Platnumz – Chacun pour soi
Hapo awali, Director Kenny ndiye alikuwa director rasmi wa Zoom Extra na alihusika kuandaa video nyingi za Diamond Platnumz.
Baada ya Kenny kuacha kufanya kazi na Diamond, Ivan ndiye amehusika kuandaa video ya Diamond ya kuitwa ‘Unachezaje’, na tangu kuachiwa kwa video hiyo, kumekuwa na tetesi kuwa huenda yeye akakaimu nafasi ya Kenny kwenye kampuni hiyo ya Zoom Extra.
Akiongea kwenye mahojiano hivi karibuni, Ivan amefunguka kuwa kila mtu ana nafasi yake kwenye muziki na kwamba anaamini kabisa Kenny ana ubora wake na hayuko pale kwa ajili ya kuchukua nafasi yake.
“Haimaanishi kwamba mimi nitachukua nafasi ya mtu yeye atabakia na nafasi yake na mimi ntabakia na nafasi yangu. Kila mtu ana makali yake. Kenny ana makali yake, Hanscana ana makali yake na mimi nina makali yangu pia. Ni kuonesha watu ni kitu gani ambacho natakiwa kufanya na kustick sehemu ambayo unadhani hii inafaa,” alizungumza Ivan.
Aidha, kupitia mahojiano hayo, Ivan alieleza kuwa alijifunza mambo lukuki kipindi anafanya kazi na Diamond Platnumz kwenye ‘Naanzaje’ amabayo ilikuwa kazi yake ya kwanza kufanya na Diamond.
RELATED: Krizbeatz – Proper Ft. Diamond Platnumz X Tekno
“Yeye Diamond ni mtu ambae amefanya video na madirectors wengi sana, wakubwa sana so anajua mistakes ambazo sisi watanzania tunakuwa tunazikosea. Mtu design kama ile akija akikwambia fanya hivi fanya hivi unakuwa unaelewa,” alizungumza Ivan.