Usomaji wa Biblia Umeimarisha Afya ya Akili katika Kipindi cha Covid19
Usomaji wa Biblia umesaidia sana kuimarisha afya ya akili za wakristo wengi duniani katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Usomaji wa Biblia umesaidia kuimarisha tiba ya akili hasa kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa corona na umesaidia kuondoa wasiwasi kuhusu maisha ya mbeleni na hii ni kutokana na tafiti za watu wa bara la ulaya.
Zaidi ya maeneo 1,123 wanaoamini ukristo, wanaoendelea kwenda kanisani na wote wenye uwezo wa kusoma Biblia kwa mwezi, imeonesha kuwa asilimia 33% ya watu wamesema usomaji wa biblia umesaidia kukukuza afya ya akili kipindi hiki cha mlipuko na wakati huo huo asilimia 28% walisema imewasaidia kuwajengea ujasiri wa kupambana na maisha yao ya kila siku, Asilimia 42% imewasaidia kuboresha tumaini lao kwa Mungu.
Katika utafiti huo watu wengi walisema kuwa usomaji wa Biblia umewasaidia kuweza kusimama tena na kupambana kwa ajili ya maisha yao ya kila siku na pia imewasaidia kutambua kuwa Mungu ni yule yule na ataendelea kubaki kuwa Mungu siku zote.
Uchunguzi huo ulifanywa na taasisi ya wakristo katika jamii ya wasoma Biblia.
“Inatia moyo kuona kuwa Biblia inawapa watu matumaini na ujasiri”.
Mwandishi “Andrew Ollerton” wa mambo yanayohusu Biblia alisema,”Biblia inaweza kusimama katika nyakati zetu za mpito(Changamoto) katika mambo magumu hasa katika nyakati zisizotegemewa”. Ollerton aliongezea kwa kusema,” Ni kama kuanguka baharini alafu ukutane na mwamba wa kujizuia (kukusaidia)”.
KATIKA TAFITI NYINGINE.
•Asilimia 84% ya wakristo wamekuwa na vipindi vya usomaji Biblia mara kwa mara.
•Asilimia 35% wamesema usomaji wa Biblia umekuwa sehemu ya maisha yao tangu mlipuko wa ugonjwa uanze.
•Asilimia 16% walieleza kuwa husoma Biblia pale tu wanapokuwa na huzuni au upweke.
•Asilimia 33% ya wakristo waliokuwa na umri kati ya 16 na 24 walieleza kuwa usomaji wa Biblia umewasaidia kupunguza upweke.
Naomi Campbell ni mama wa watoto wawili huko ulaya, Aliiambia jamii ya usomaji wa Biblia kuwa kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa yeye alijipatia nguvu kutoka katika kitabu cha Isaya 61:3.
“Umenipa vazi la sifa badala ya roho nzito”. Alieleza kuwa maisha yake yalikuwa na changamoto nyingi lakini tukiachana na yote Mungu ametupatia nafasi ya kuuona uzuri wake na uumbaji wake katika maisha yetu. Aliendelea kusema kuwa mstari huo umeujaza ndani ya nafsi yake kipindi chote cha kujifungia ndani (lockdown), Na akamalizia kwa kusema kuwa mstari huo umemshangaza mara zote.
Chanzo: christianheadlines.com